MAFINDO FINDO (TONSILLITIS)
Mafindo findo (Tonsillitis) Nimaambukizi yanayosababishwa na aina tofauti tofauti ya vimelea vya maagonjwa ikiwemo bakteria,virusi,fangasi.ambavyo husababisha kuvimba kwa findo (Tonsil)
Uenezwaji/Maambukizi
Mafindofindo huenezwa kwa njia ya
Hewa
Kwa kupiga chafya
Kwa kukohoa
Kugusa majimaji yenye vimelea
Kubusu
Kubadilishana mate (kunyonyana ndimi)
Kubadilishana vinywaji
Dalili/Ishara za Tatizo
Maumivu
Hutokea sehemu yenye uvimbe pamoja na maeneo ya masikio
Wakati wa kumeza kitu chochote
Mwili mzima kuhisi.
Mwili kuchoka
Kuhisi homa (mwili wa moto)
Kutetemeka
Kuhisi uchovu
Pua
Mafua (makamasi kuteremka)
Pua kuziba
Kupata shida ya kupumua
Masikio na mdomo
Kupata shida ya kusikia na kuongea
Kupumlia mdomo
Dalili zingine
Shingo kuvimba
Kutokwa na machozi
Kukosa hamu ya kula
Kuvimba mitoki
Mafindo findo hutibika pale upatapo matibabu sahihi.
Njia za kujitibu mwenyewe bila kwenda hospitali zipo .
Unaweza tumia njia hizi kutatua tatizo la mafindo findo.
Kumbuka. Kama Moja ya njia hizi haitafua dafu tafadhali wahi kupata ushari wa daktari.
Maji ya Moto na asali tumia Kama unavyojua andaa chai
Maji ya Moto na chumvi fanya Kama hapo juu.
Muone mtalaam wa afya kwa ushauri wa dawa gani sahihi ya kutumia.
Kama mafindo findo haikutibika kwa muda wa mwezi unahitaji uchunguzi zaidi wa kitalaam.
Pia Kama mafindo findo haijafanikiwa kutibika unahitaji tiba ya Upasuaji kuziondoa.
Jamani nahisi kuchanganyikwa mwanangu anaumwa
ReplyDelete