Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

Kifafa cha mimba

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaohusiana na msukumo mkubwa wa damu (high blood pressure) kipindi cha Mimba au ujauzito
Kifafa cha mimba ni tatizo ambalo linasababisha vifo vyingi sana vya mama wajauzito na watoto wakiwa tumboni.

Kuna Aina mbili za kifafa cha mimba
Kifafa cha mimba cha awali (pre eclampsia) na kifafa cha mimba kamili (Eclampsia).

Vitu vinavyoweza pelekea mtu kuwa kwenye hatari ya kupata kifafa cha mimba ni kama vile.
  • Umri chini ya miaka <18
  • Kuwa na historia ya tatizo la kifafa kabla ya ujauzito
  • Kuwepo na historia ya kifafa cha mimba mwenye familia
  • Ujauzito wa mapacha au kuwa na historia ya mapacha kwenye familia
  • Kuwa na historia ya kifafa kwenye ujauzito wa Mara ya kwanza
  • Ujauzito wa Mara ya kwanza
  • Kubadilisha badilisha wanaume
  • Mama mwenye tatizo la kisukari
  • Mama anayevuta sigara
  • Ulevi

Dalili.
  • Maumivu ya chembe ya moyo
  • Kuwa na msukumo mkubwa wa damu.
  • Kuvimba na kubonyea kwa miguu(Pitting Oedema).
  • Kuwa na protini kwenye mkojo.
  • Kizunguzungu
  • Kupata degedege
  • Macho kuoana giza.
  • Kichwa kuuma

MADHARA YA KIFAFA CHA MIMBA.
  • Mama mjamzito anaweza kupoteza maisha yeye na mtoto wake.
  • Kuzaa mtoto mfu.
  • Mama kuendelea kuwa na tatizo la kifafa maisha yako yote. (Epilepsy)
  • Mama kuendelea kuwa na tatizo la shinikizo la damu la kupanda.(High blood pressure)
  • Kuzaa mtoto mwenye uzito
    pungufu.

Uchunguzi
  • Mama atachunguza mkojo kuangalia protini
  • Mama atapimwa kuangalia msukumo mkubwa wa damu Mara kwa Mara
  • Atapimwa vipimo vingine  ninavyo endana na tatizo lakwe alilonalo au linalopelekea kupata kifafa cha mimba
Matibabu
  • Mama atashuriwa kuzaa au kuzalishwa pale mimba itakapofika wiki 37
  • Mama atashauriwa kulazwa au kupumzika
  • Mama atapewa dawa za kuzuia kifafa
  • Mama atapewa dawa za kupunguza msukumo mkubwa wa damu

Kwa ushauri na maelekezo mengine wasiliana nasi kwa WhatsApp no 0684127127

Kama una swali Unaweza uliza kwa hapa chini au kwa namba ya WhatsApp niliyotaja hapo juu 

Post a Comment

Translate