NJIA ZA UZAZI WA MPANGO.
UZAZI WA MPANGO: Ni njia zinazotumiwa na mtu au wanafamilia kwa ajili ya kupanga uzazi, idadi ya watoto wanaotaka kuzaa, nalini wazae watoto.
FAIDA ZA UZAZI WA MPANGO (KUPANGA UZAZI)
Husaidia kuzuia Mimba isiyotarajiwa.
Mama atapata muda wa kutosha kumlea mtoto na kurejesha afya ya mama
Husaidia mtoto kunyonya maziwa ya mama kwa muda mrefu na kumsaidia kupata afya ya kimwili na kiakiri.
Husaidia wanafamilia kupata muda wa kutosha wa kutunza mtoto na kupatia mahitaji muhimu kwa ukuaji wake.
Hupunguza vifo visivyotarajiwa
MAKUNDI YA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO.
Kuna makundi matatu(3) ya njia za uzazi wa mpango.
Njia za Muda mfupi
Kondomu (kike na kiume)
Sindano
Vidonge
Kuhesabu kalenda
Kumwaga nje (Kuchomoa uume)
Njia za Muda mrefu
Vipandikizi
Lupu (kitanzi)
Njia za Kudumu
Mwanamke kufunga kizazi
Mwanamme kufunga kizazi
KONDOMU.
Husaidia Mimba kwa kuzuia mbegu za kiume kuingia kwenye uke wa mwanamke.
Kuna kondomu za kike na za kiume.
FAIDA ZA KONDOMU
Huzuia Mimba
Huzuia magonjwa yaambukizwayo kwa njia ya ngono (kujamiana) kama ukimwi,kaswende,kisonono kama itatumiwa ipasavyo.
Ni Rahisi kutumia na hupatikana kirahisi.
Maudhi madogo madogo
Husababisha kuwashwa kwa ngozi.
KUMWAGA/KUMWAGA NJE(KUCHOMOA UUME)
Wakati wa kufanya tendo la ndoa (kujamiana) mwanaume anamwagia shahawa nje ya uke.
Njia hii haina madhara yoyote isipokuwa mtumiaji wa njia hii kama akiwa mzembe shahawa zikamwagikia ndani wakati anajiandaa kutoa ume nje Kuna hatari ya kupata ujauzito.
FAIDA ZA NJIA HII.
Huzuia Mimba kwa kiasi kidogo sana.
HASARA
Haizui maambukizi ya magonjwa yasababishwa na kujamiana.
Watu wengi hawawezi njia hii hujisahau na kujikuta amemwagia ndani.
NJIA YA VIJITI. Imeelezwa kwenye post inayofata
Post a Comment