Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

ZIFAHAMU SABABU ZINAZOPELEKEA MWANAMKE KUTOKWA NA DAMU WAKATI AU BAADA YA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA.

Kuna sababu kadha wa kadha zinazo mpelekea mwanamke kutokwa na damu wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Damu inayotoka katika kipindi hiki Inaweza kuwa imejumuisha zifatazo za sehemu ya uzazinwa mwanamke
              •> Uke
             •> Shingo ya kizazi
             •> Mji wa mimba
             •> Mirija ya hajandogo
Kwa hiyo inategemea shida iko sehemu gani
            
Moja ya sababu hizo ni kama.
Kuwa na maambukizi ya mfumo wa uzazi kwa kitalaam unaitwa Pelvic inflammatory Disease (PID) Au Magonjwa yasababishwayo au yaambukizwayo kwa njia ya kujamiana. Kama
                  •> Kisonono (Gonorrhoeae)
                  •> Chlamydia Trachomatis n.k.
                  •> kaswende
Ukavu uke hii ni kuwa unakuta  mwanamke anakuwa na uke kuwa mkavu ambapo inapelekea kupata michubuko wakati wa tendo na baada ya tendo kupata maumivu makali na kufatiwa na damu Kutoka
   
  Je vitu gani vinapelekea mwanamke kuwa na uke mkavu.
              •> Kupungua kwa homoni Aina ya estrogen ambayo ninakazi ya kuwa kama kilainishi.
              •> Hofu inapelekea Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa
              •>  Matumizi ya vitu kama sabuni, pafumu, lotion na vitu vingine  kuoshea  uke husababisha  kuondosha mazingira asili ya uke.
              •> Kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa pia kupelekea kufanya uke kuwa mkavu na kupelekea kutokwa na damu wakati wa tendo.
Uke kuumia (vaginal damage)  kwa sababu kadha wa kadha kama :-
            •> Kuchanika msamba (tears) wakati wa kujifungua, kama sehemu iliyoshonwa haijapona vizuri Inaweza pelekea mama kutokwa na damu wakati wa tendo.
            •> Uke kuwa mkavu kutokana na msuguano wakati wa tendo pengine  kwa sababu ya kukosa maandalizi mazuri hupelekea  mwanamke kutokwa na damu.
Uwepo wa viuvimbe /saratani kwenye mji wa mimba . Huweza pelekea kutokwa na damu wakati wa tendo au baada ya tendo
Kuwepo na uvimbe kwenye shingo ya kizazi pia niasababisha  mwanamke kutokwa na damu punde au wakati wa tendo la ndoa.
Uwepo wa saratani (kansa) kwenye mji wa mimba au shingo ya kizazi humpelekea mwanamke kupata shida ya kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa au baada.
Mwanamke kuwa na historia ya kupata ajari( Trauma) inayohusiana mji wa uzazi  kwa ujumla kama haikupona ipasavyo inapelekea mwanamke kutokwa na damu wakati au baada ya kushiriki tendo la ndoa.
Mwanamke anapokoma hedhi pia anakuwa anapata shida ya kutokwa na damu ukeni
Watu gani Wapo kwenye hatari ya kupata shida hii
          • Mwenye kansa /saratani ya kwenye shingo au kwenye mji wa uzazi
          • Kuwa na wanaume wengi (michepuko mingi kwa mwanamke)
          • Mwanamke anayeelekea kukoma hedhi.
          • Wanawake wenye tabia ya kujiosha uke Mara kwa Mara (douching)
          • Kuchanika msamba wakati wa kujifungua.
Matibabu ya tatizo inategemea na chanzo cha tatizo ni nini.
Unazuiaje Maumivu na damu Kutoka
          •  Tumia vilainishi
          •  Punguza wenza (Michepuko)
          • Tibu chanzo cha tatizo.
          • Kuwa na maandalizi ya kutosha wakati wa tendo la ndoa pia Fanya tendo kistaarabu.
         
                       • Well organization & Wmedsclinic
                       •0743127127/0684127127

Post a Comment

  1. Nafanyaje ili nijue siku hatari kwa mpenzi wangu kubeba mimba,

    ReplyDelete

Translate