Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO

vidonge vya uzazi wa mpango. Ni vidonge vinavyotumiwa na wanawake wengi kwa kumlinda asipate mimba pia vinatumika kama njia ya kutibu wanawake ambao wanashida ya homoni.
Ni njia  ya Muda mfupi
Zina homoni zinazofanana na homoni zilizopo mwilini mwa mwanamke.
Kuna aina  mbili za homoni ambazo zilizopo ambazo ni estrogen na progesterone  (combined oral contraceptive) Kifupi (COC)

Zinafanyaje kazi

•  Huzuia yai la kike kukomaa kwa ajili ya Kuja kurutubishwa na mbegu ya kiume
• Hufanya mazingira yasiyo rafiki kwenye mji wa mimba kwa mbegu za kiume kupenya kwenda kurutubisha yai la kike.

Faida za njia hii

• Anatumia  mtu yoyote baada ya kupata ushauri Kutoka kwa daktari
• Huzuia mimba
• Hurekebisha mzunguko wa hedhi
• Kurudisha Hali ya homoni ya awali ndani ya muda mfupi.
Vidonge hivi vinatumika kila siku kidonge kimoja (1) bila Kusahau ndani ya siku 28
Zingatia muda unatumia kila siku bila kupishanisha

Maudhi madogo madogo ya njia hii

• Kichwa kuuma
• Kizunguzungu
• Kichefuchefu
• Mzunguko wa hedhi kubadilika
• Matiti kuuma

Mtu yupi  anatumia  njia hii

• Baada ya kufikisha miezi 6 baada ya kujifungua na wakati huo ulikuwa kunyinyesha mtoto.
• Inafaa kwa mwanamke yoyote baada ya kuongea na kushauriana na daktari

Nani haruhusiwi kutumia njia hii

• Historia  ya saratani ya matiti
• Kisukari
• Shindikizo kubwa la damu (presha)
• Homa ya ini
• Tatizo la damu kuganda
• Chini ya miezi 6 baada ya kujifungua kama unanyonyesha.
• Kama unatokwa na damu ukeni.

Dalili mbaya za vidonge kwa mtumiaji akiziona awahi kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.

• kifua  kuuma sana
• Shida ya kuona (macho)
• Maumivu makali ya tumbo
• Maumivu kamali ya miguu


Progestin only pills (pop)

Njia nyingine ambayo ina homoni moja ambayo inaitwa progestin
Njia hii inafanya  kazi kama  (cos) kama nilivyo eleza hapo juu.

Maudhi madogo madogo ni kama

• Kubadilisha mzunguko wa hedhi
• Kupunguza macho kuona
• kupata hedhi kama matone  marine (spots)
• Damu kutotoka kabisa
• Damu Kutoka nyingi
• kichwa kuuma
• Kichefuchefu

Mwanamke yupi  hashauriwi kutumia

• Tatizo la damu kuganda
• Kama unatumia dawa za kifua kikuu (TB)
• Kama kuna damu zinakutoka ukeni bila kufahamika chanzo.
• kama una Tumia dawa za Maambukizi ya virusi vya ukimwi.
• Mwenye historia ya kansa ya matiti
Matumizi ni kama (coc)

Karibu kwa maswali 

Post a Comment

Translate