Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

Je wewe ni mjamzito? Fahamu mambo muhimu kuhusu afya ya mama mjamzito:

1. Wakati wa ujauzito, unaweza kusikia uchovu mkubwa au usingizi. Mara nyingi uchovu huu upo katika miezi mitatu ya awali
2.Kama mjamzito, jitahidi kupumzika na kuweka miguu juu kila unapoweza na ulale na mito kati ya miguu yako na ulale mapema
3. Kizunguzungu wakati wa ujauzito ni jambo la kawaida na inaweza kusababishwa na msukumo wa damu (presha) kushuka
4. Kizunguzungu wakati wa ujauzito huweza kusababishwa na sukari ktk damu kushuka, upungufu wa madini chuma mwilini, upungufu wa maji mwilini
5. Kusimama ghafla pia huweza kupelekea mama mjamzito akasikia kizunguzungu. Inashauriwa kama mjamzito, usimame taratibu
6. Je wajua mama mjamzito anaweza kupata kisukari kinachosababishwa na ujauzito? Hujitokeza katika miezi ya 4 mpaka 6
7. Kwa akina mama wajawazito maji ni muhimu kuunda kondo ya nyuma na kuboresha mfuko wa uzazi ili mtoto apate virubutisho muhimu
8. Je unajua mstari mweusi upo mwilini mwa mama mjamzito kwenye tumbo katika hali ya kawaida kabla ya ujauzito lakini hauonekani sana? Huitwa Linea NIgra
9. Uvutaji sigara wakati wa ujauzito huweza kupelekea mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake (mtoto njiti) au kuzaliwa na uzito mdogo
10.Uvutaji sigara wakati na baada ya ujauzito pia huweza kupelekea mtoto kufariki ghafla. Sigara ina kemikali zaidi ya 4,000
11. Nini hupelekea mishipa kutuna wakati wa ujauzito? Kadri mtoto anavyokua, presha huongezeka katika mfuko wa uzazi na mishipa
12. Una uwezekano mkubwa zaidi wa mishipa ya damu kuvimba sana kama ni mjamzito na umebeba zaidi ya mtoto mmoja tumboni
13. Ni vyema kupumzika na kuweka miguu juu mara kwa mara wakati wa ujauzito ili kupunguza mishipa kuvimba sana
14. Je wajua kuwa wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua, akina mama huweza kupata mfadhaiko (postpartum depression)?
15.Ni muhimu kwa familia kuwa makini na kutomwacha mama mjamzito au mwenye mtoto mchanga ambaye ana huzuni au mawazo bila msaada wa kitaalam
16.Takriban 25% ya akina mama hutokwa na damu kidogo uukeni wakati wa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo.
17.Ukitokwa na damu nyingi na maumivu ya tumbo wakati wowote wa ujauzito, kamwone mtaalam mara moja!
Ufahamu ukuaji wa mtoto akiwa tumboni na nini ufanye  uonapo hali isiyo ya kawaida 
Kwa Maelezo zaidi /Ushauri kuhusu ujauzito wako usisite kuwasiliana nasi kwa kuandika ujume wako /swali hapo chini.
Pia waweza wasiliana nasi kwa namba zifatazo kupitia
      WhatsApp 0684127127 - 0762986021
                Ahsante

Post a Comment

Translate