Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

TATIZO LA KISUKARI AINA,CHANZO,DALILI,MADHARA YAKE NA MATIBABU YAKE 


Kisukari ni ugonjwa wa kimetabolisim (ikimaanisha ni matokeo ya ufanyaji kazi wa mwili) unaotokea baada ya shida kwa mwili kupangilia utolewaji wa kichocheo ama hormone ya insulin. Hivo dalili za Kisukari ni matokeo ya kupanda kwa kiwango cha sukari kwenye damu kunakotokana na kufeli kwa kichocheo hiki cha insulin kufanya kazi, mpenzi msomaje hapa napenda uelewe kwamba kiwango cha sukari kwenye damu kitaaanza kuleta athari endapo kiwango cha insulin kinachomwagwa ni kidogo yaani hakitoshelezi kutokana na seli za beta zilizopo kwenye kongosho ambazo hutengeneza kichocheo hiki kuwa na hitilafu, sababu ya pili ni  pale mwili unakuwa hausikii uwepo wa insulin kwenye damu kitaalamu tunaita INSULINI RESISTENCE., yaani kongosho linamwaga insulin kwenye damu lakini kiwango cha sukari bado kipo pale pale hapa ndipo tunapata kisukari cha ukubwani. Hii ni hatua mbaya kufikia ambapo wagonjwa wengi hukosa tumaini na hukata tamaa katika kutafuta dawa ya kisukari cha kupanda. Huhitaji kufikia huko fuata lishe sahihi utaishi bila Kisukari.
Aina Za Kisukari
Kuna aina kuu 2 za Kisukari, aina ya kwanza ambayo Kisukari cha utotoni na aina ya pili ya Kisukari ambacho ni Kisukari cha ukubwani.

1.  Kisukari Cha Utotoni
Aina hii ya Kisukari huanza pale mtoto anapozaliwa hadi kufkia umri wa miaka 18 au 20, husababishwa na mpambano kati ya kinga ya mwili dhidi ya seli za beta ambazo hutengeneza homoni ya insulin (homoni inayorekebisha kiwango cha sukari kwenye damu), sasa mpambano huu hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa insulini ama kukosekana kabisa kwa insulin kwene kongosho, na kwasababu miiili yetu imeubwa kutumia insulini wagonjwa hawa huhitaji kudungwa sindano za insulin kila siku ili kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

Dalili Za Kisukar Cha Utotoni ( Type 1 Diabetes)

Wagonjwa wenye aina hii ya Kisukari huwa wamekonda na kudhoofu sana afya zao   Seli za kutengeneza kichocheo cha insulin zinakuwa zimeangamizwa kwa kiasi kikubwa kutokana na mpambano na kinga ya mwili. Kiwango cha insulin kwenye damu huwa kipo chini sana kutokana na uwezo mdogo wa kongosho kutengeneza insulin.

Kisukari Cha Ukubwani (Type 2 Diabetes)
Aina hii ya Kisukari nafahamika sana na imekuwa janga la dunia nzima likiathiri mamia ya watu kila siku. Kinyume na Kisukari cha utotoni, aina hii ya Kisukari husababishwa na kiasi kikubwa cha insulin kwenye damu. Hivo ukiwa na Kisukari cha ukubwani ni kwamba insulin iliyo nyingi kwenye damu na mwili hauwezi kuitumia vizuri hali hii kitalamu ni insulin resistence, ama kongosho yako inatengeneza insulini nyingi lakini imezidiwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu. Kupanda kupita kiasi kwa kiwango cha insulin kwenye damu huweza kuletekeza ama kupelekea matatizo mengine ya kiafya  kama.
• Kiharusi/Stroke na matatizo mengine ya utendaji wa ubongo kama Alzheimer
• Kupanda kwa shindikizo la damu
• Magonjwa ya viungo arthritis
• Kupungua uwezo wa Kuona na hatimaye kuwa kipofu.
• Kitambi na Uzito mkubwa
• Kufeli kwa figo
• Kurundikama kwa Mafuta mabaya kwenye viungo muhimu kama
•  Ini
• Saratani
• Upungufu wa nguvu za kiume
Matatizo ya uzazi kwa wanawake kama ugumba na uvimbe na
• Matatizo ya upumuaji /kupumua kwa shida na Mzio (aleji).

Dalili Za Ugonjwa Wa Kisukari Aina Ya Pili(Kisukari Cha Ukubwani)
• Kupumua kwa shida,
• Aleji
• Vidonda kutoponamapema, 
• Maambukizi ya mara kwa mara.
• Kuongezeka uzito kusiko kawaida pengine hata bila kubadili lishe yako.
• Kupata kiu ya mara kwa mara na mdomo kukaukaMwili 
• Kujisikia mechoka muda mwingi na kupata ganzi kila mara.
• Kupata athari za neva na kusababisha maumivu ya viungo na kutetemeka kwa miguu na mikonoKupungua kwa uwezo wa kuonaKupata njaa na kujiskia kula mara kwa mara, hata kama umekula hivi karibuniKupoteza uwezo wa kufatilia mambo na kujitambua (consciousness) .

Kumbuka kwamba siyo lazima uone dalili zote hizi ndipo unaashiria umeanza kuugua Kisukari, unaweza kujipima mwenyewe na kuchukua hatua ya kufika hospitali upate ushauri ili upunguze hatari ya kuugua Kisukari.
Hivo magonjwa haya huambatana na tatizo la Kisukari na kadri ugonjwa unavokomaa na kufkia hatua mbaya ndivyo magonjwa haya ambatanishi yanavojitokeza Zaidi, najua unaweza kuwa ni muhanga wa ugonjwa huu na umeteseka kwa miaka mingi umetumia madawa mengI bila mafanikio, napenda kukupa tumaini kuwa suluhisho lipo, ni kurekebisha lishe yako tu na kutumia virutubisho muhimi. Unachotakiwa ni kufuta imani ulopewa hapo wali kwamba kula mboga za majani kwa wingi na matunda, maana elimu hiyo haijakusaidia na bado unaumwa na kuteseka na Kisukari.

Nini Chanzo Cha Kisukari Cha Ukubwani?

Kwanza kabisa ni vyema kufahamu kwamba ugonjwa wa Kisukari siyo ugonjwa wa kuwa na sukari nyingi hapana, Kisukari ni ugonjwa wa homoni, homoni ya insulin, kumbuka kwamba mwili unahitaji kiwango kidogo tu cha glucose kukibadilisha kuwa nishati ili kuendesha shuguli zake, kiwango kingine kinachozidi huwa hakipotei bali huhifadhiwa katika seli za mwili kwenye mfumo wa mafuta, hivo kazi ya insulin ni kusukuma sukari iliyozidi kwenda kwenye seli ili ibadilishwe kuwa mafuta. Sasa inapotokea mwili hausikii uwepo wa insulin kwenye damu yaani insulin inamwagwa lakini kiwango cha sukari kwenye damu kipo pale pale hao ndipo hatari ya kuugua Kisukari cha ukubwani huanza.
Sasa ni wakati wa kutambua kwamba aina ya chakula unachokula kinachangia kwa kiasi kikubwa kupata magonjwa haya kama Kisukari na uzito mkubwa,vyakula kama wanga na sukari hupandisha insulin kwenye damu kwa kasi sana huku vyakula vya protini na mafuta vikithibitika kupandisha insulin kwa kiasi kidogo sana. Kula wanga na sukari nyingi na kufanya mazoezi sana haikusaidii kuepuka magonjwa haya ya Kisukari na uzito mkubwa badala yake kula vyakula vya mafuta kama parachichi, samaki, nyama, mayai , nazi na mboga za majani kwa wingi muhimu.Na swali kubwa ninalopata ni kwamba “lishe ya mtu mwenye kisukari ni ipi? basi nashauri fuata ?/FANYA YAFUATAYO ILI USIUGUE KISUKARI CHA UKUBWANI (Type 2)

Punguza Wanga Na Sukari
kwanini tunakushauri upunguze wanga na sukari?
Unapokuwa umepunguza wanga na sukari au kuacha kabisa ulaji wa vyakula vyenye wanga nyingi, mfano mikate,ugali,wali,tambi nk na hakikisha kitendo hicho kiendane na kuongeza kiwango cha mafuta na vyakula vya protini mwilini mwako katika lishe yako. Hii itaufanya mwili wako kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili ya kwanza kujitengenezea nishati. Na viungo vya binadamu kama Ini na figo vinapokuwa vinatumia mafuta kuzalisha nishati ya mwili hutenegeneza viini vya nishati viitwavyo ketone bodies ambavyo hivi ndivyo hutumiwa na seli za mwili kujitengenezea nishati kwa wingi.
Hivyo basi unapokuwa unajizuia kutumia vyakula vya wanga mwili wako utatumia karibia siku 5 hadi wiki kuanza kutumia mafuta kama nishati ya mwili na hicho kitendo tunaita Keto adaptation . Ningependa kusema kwamba Keto adaptation ni ile hali mwili wako kujenga mazoea ya kutumia mafuta kama chanzo cha nishati ya mwiliala ya sukari hapo ndipo utaanza kuona mabadiliko katika mwili wako makubwa sana na utaondoa hatari ya kuugua kisukari cha ukubwani (type 2 diabetes).
Utakuwa unajisikia mwenye nguvu na unatashangaaa dalili mbalimbali zilizokuwa zinakusumbua zinapotea hii ni kwa sababu ya uwezo mkubwa wa ketone bodies katika mwili wako dhidi ya glucose.
Sote tunajua kwamba ulaji wa vyakula vya wanga kwa wingi na vyakula vyenye sukari nyingi vinaongeza kiwango cha sukari kwenye damu Zaidi ya kiwango ambacho mwili wako unaweza kuhimili.
Mfano, Kiwango cha kawaida cha sukari kinachohitajika mwilini mwako ni kijiko kimoja cha chai, hiki ni kiwango ambacho hakiwezi kukuletea matatizo. Basi kama binadamu anaishi kwa sukari inayokadiriwa kuwepo kwenye damu kama kijiko kimoja tu cha chai. Unywaji wa soda moja unaweza kuongeza Zaidi ya vijiko 10 hivyo basi mwili wako unakuwa unashindwa kuhimili sukari iliyozidi. Na ulaji wa Baga inakadiliwa kuwa baga moja ya kati inaweza kutoa sukari Zaidi ya vijiko 16 kwenye damu. Swali la kujiuliza mwili unapeleka wapi sukari iliyozidi wakati miili yetu inahitaji sukari kiwango kidogo sana kama kijiko kimoja tu kuishi?
Mwili hutengeneza maji kutoka kwenye seli za  kongosho ziitwazo beta seli,maji haya ni homoni iitwayo INSULIN, Kazi kubwa ya insulin ni kutunza glucose hii katika damu kwa matumizi ya baadae, na inatunza katika kiasi maalumu katika mfumo wa Glycogen na kiasi kikubwa katika mafuta. Na hivyo basi mafuta haya huhifadhiwa katika sehemu mbalimbali kama tumboni, shingoni, mikononi, kifuani, kiunoni nk. Na mafuta haya huhifadhiwa katika mfumo wa TRYGLYCERIDES ambayo haya ni miongoni vya mafuta mabaya mwilini mwako. Sasa mtu anayekwambia wanga nyingi katika chakula chako ni salama anakudanganya kwa kiasi kikubwa kwani tunaona jinsi gani ulaji wa kiwango kingi cha vyakula vya wanga na sukari vinavyo sababisha sukari kupanda kupita kiasi na insulinkuanza kuhifadhi katika mafuta.
Fahamu kuanzia sasa kwamba adui wako mkubwa siyo fat kama ulivofundishwa na kusoma, adui wako ni wanga na sukari. anza kubadili mfumo wako wa maisha na utashangaa jinsi kisukari cha ukubwani itakavokuwa historia kwako pamoja na magonjwa mengine kama upungufu wa nguvu za kiume, kuvurugika kwa homoni, kitambi+uzito mkubwa, na mengine mengi.

Fanya Vipimo Mara Kwa Mara
Wagonjwa wengi wa Kisukari huwa ni vigumu kugundua tatizo mpaka pale linapoanza kuleta athari kubwa. Umuhimu wa kupima ni kugundua tatizo mapema na kuanza kuchukua hatua ili kuzuia hatari kubwa. Hivo ni muhimu kufatilia matukio kama kuongezeka kwa shinikizo la damu na kuongezeka uzito na kiwango cha sukari kwenye damu.

Kisukari kinatibika kabisa 
Karibu tukutatulie changamoto ya kisukari
TUPIGIE SASA: 0743127127 | 0684127127
WhatsApp: 0684127127
FB page: Well Clinic | Afya
Instagram :Well Clinic
Blog : well Clinic

Post a Comment

Translate