Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

KARIBU AFYA KIGANJANI MWAKO
        



HEDHI ni hali ya mabadiliko ya mwili kwa mwanamke ambapo  kila mwezi mwili hutoa yai moja kwa lengo la kurutubishwa kwa utungaji wa Mimba (ujauzito)
Kuna Aina kadha wa kadha za hedhi kulingana na siku ambazo mwanamke atatoa damu
      Mzunguko wa siku  28 ndio mzunguko wa kawaida kabisa ambao wanawake wengi huingia
      Mzunguko wa siku  21 ni mzunguko ulio mdogo  kuliko yote
      Mzunguwa wa siku 30 ni mzunguko wa siku
      Mzunguko wa siku 45
Ukomo wa hedhi ni umri gani ?

Wanawake wengi wanakuwa na ukomo wa hedhi (menopose) kati ya miaka 45 -55 na wengine kupata ukomo huo wakiwa chini ya miaka 45 na hii husababishwa na sababu kadha wa kadha  ikiwemo
     kuridhi kutoka kwa familia( mama mzazi)
     Matumizi ya madawa kadha wa kadha (matibabu)
     Upasuaji unao husisha via au mfumo wa uzazi
     Matatizo ya homoni 


     Kuugua
Ni kwani nini mwanamke anapata kuwa na mzunguko usio wa kawaida (abnormal menstral)
    

SABABU ZA MSINGI ZINAZOWEZA PELEKEA MWANAMKE KUPATA DAMU NYINGI WAKATI WA HEDHI.

Sababu zifatazo zinaweza kuwa chanzo au sababu za kupata mvurugiko/kukosa hedhi kabisa
1.Mvurugiko wa homoni (Hormonal imbalance)
Ili hedhi iende Sawa kuna kuna homoni zinazohusika kuweka Sawa mwenendo sahihi wa hedhi ambazo zinachochea mpangilio mzima wa hedhi.
Homoni hizi ni  oestrogen na progesterone hutakiwa kuwa katika usawa ili viweze kufanya kazi yake ipasavyo, na hii hupelekewa na  Matumizi ya vichocheo katika kupanga uzazi kama (vijiti/contraceptive pills) huweza kubadili Hali ya vichocheo na kusababisha hali hiyo kutokea hupelekea  ukuta wa mfuko wa mimba hutoa damu nyingi isiyokawaida, ikiambatana na mabombe
2. Matatizo ya ovari.

Ovari ni sehemu inayohuseka katika uandaaji wa yai na baadae kutolewa likiwa kamili kuingia katika mirija ya fallopia  kwa ajiri ya kurutubishwa tayari kwa safari kuelekea mfuko wa kizazi kama kijusi
Kama ovari zitashindwa kutoa mayai basi tatizo huwa ni upungufu wa kichocheo kiitwacho progesterone hicho yai haliwezi kutoka kwenye ovari na hali hii husababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.
3. Kuwepo kwa Uvimbe kwenye sehemu ya kizazi (Myoma/Fibroids)

Fibroids/ myoma siyo saratani bali ni uvimbe unaojitokeza karibu na kizazi unajulikana kama  (benign), ambayo hutokea katika umri wa uzazi.
Kwanini benign hutokea ?
Husababishwa na matumizi ya njia za uzazi wa mpango ambavyo  huharibu usawa wa homoni au vichochezi na huweza kusababisha damu nyingi kutoka wakati wa hedhi.
4. Vimbe ndogondogo kwenye kizazi.
Huwa ni vimbe ndogo sana katika mfuko wa uzazi.
Hutokea kwa wanawake katika umri wa kuzaa kutokana na  vichocheo kuongezeka.
5. Magonjwa ya kurithi.
Mwanamke akiwa na Matatizo ya damu kutoganda kutokana na hii husababishwa na ukosefu wa vigandishi vya damu. Hupelekea mtu kuvurugika kwa hedhi.
6. Kuugua au Matatizo ya kiafya.
Kuna magonjwa  mengi sana yanayo weza pelekea mwanamke kubadilisha mvurugiko wa hedhi kama vile
Maambukizi katika njia ya kizazi kama Pelvic Inflammatory Diseases(PIDs),Maambukizi sugu ya magonjwa ya zinaa (kisonono,kaswende n.k)
7. Matumizi ya madawa makali kwa muda mrefu
Matumizi ya dawa Kali kwa muda mrefu wakati wa kutibu magonjwa  kadha wa kadha hupelekea mwanamke kuharibika na wakati mwingine kukokosa hedhi kabisa
8. Kuwa na mawazo / stress kupitiliza kiasi

Je nani yuko hatarini kukumbwa na hali hii?
Makundi yafuatayo yako katika hatari ya kukumbwa na tatizo hili.
1. Wale waliovunja ungo hasa mwaka mmoja wa kwanza
2.Wanawake wanaokaribia ukomo wa hedhi kati ya miaka 40-50 wako hatarini katika mabadiliko ya vichocheo.

ZIJUE DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO HILI (Menorrhagia)
1.    Kutumia peds moja ama zaidi kila  saa moja  kwa mfululizo wa masaa kadhaa ikiambatana na maumivu makali ya tumbo ama  laa
2.    kuamka usiku mara kwa mara kubadilisha ped 
3.    Damu kutoka nyingi zaidi ya  siku nne hadi saba isivyo kawaida
4.    Kutoa mabonge ya damu wakati wa  hedhi zaidi ya siku moja.
5.    Kutoshiriki shughuli za kila siku kutokana na damu nyingi kutoka
6.    Dalili za kuishiwa damu, kama kuchoka, ama kupumua kwa shida.

MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA ENDAPO HATUA MADHUBUTI HAZITACHUKULIWA.
1.  Upungufu wa madini  ya iron na folic acid ambayo ni madini muhimu katika damu ambapo husaidia katika kubeba hewa ya  oksijeni, kukosekana ama kupungua  kwake maisha  huwa  hatarini.
2.   Maumivu makali wakati wa hedhi ambayo wakati mwingine  huhitaji  kutumia dawa za kutuliza maumivu.
3.   Kupata upungufu wa damu
4.  Kwa mjamzito ambaye Alikuwa na tatizo la kutoka na damu kwa kipindi cha nyuma kabla ya kushika ujauzito inapelekea mtoto
      kufia tumboni
      Mama kupoteza maisha
      Ujauzito kutoka
     
Je nini kifanyike kutatua tatizo?
   Ili kupata majibu ya tatizo Tafadhali unapaswa kugharamia kwa kulipia kiasi cha Tsh.2,000/= tu
Kwa M- pesa namba 0768489884
Ahsante
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

Translate