Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

 Tatizo la Mafua sugu chanzo, dalili zake na Tiba yake
Mafua ni ugonjwa wa kuambukiza unaojulikana pia kwa jina lenye asili ya Kiitalia influenza (yaani "athari") na kwa kifupi chake "flu". Kwa Kiswahili unaitwa mafua  huasambazwa kwa njia tofauti tofauti.
Ugonjwa wa mafua unaweza kusababisha hali ya kupiga chafya mara kwa mara, kutokwa na makamasi mepesi au mazito puani, kikohozi, homa kali, na kuziba kwa pua na wakati mwingine maumivu makali ya kichwa
Mafua yanaweza kuwa moja ya sababu kubwa inayofanya watu wengi kushindwa kwenda kazini, katika shughuli mbalimbali za uzalishaji au kuhudhuria shuleni na kwenda kutafuta msaada wa kitabibu hospitalini.
Ingawa dalili za mafua siyo kali sana na hazidumu kwa zaidi ya majuma matatu, Shirika la Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa la Marekani (CDC) linasema kuwa, kila mwaka mafua husababisha kupotea kwa siku milioni 22 za mahudhurio shuleni nchini Marekani.
      
     Katika utafiti wao Fendrick AM, Monto AS, Nightengale B na Sarnes M uliochapishwa katika jarida la kitabibu la Archival of Internal Medicine toleo la 163 mwaka 2003, walibaini kuwa mafua yanaweza kusababisha mzigo mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi.
    Utafiti huo uliohusisha kaya 4,051 huko Marekani, ulionyesha kuwa takribani dola bilioni 40 za Marekani hupotea kila mwaka kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua yatokanayo na virusi vya mafua.
Ugonjwa wa mafua unaweza kusababisha hali ya kupiga chafya mara kwa mara, kutokwa na makamasi mepesi au mazito puani, kikohozi, homa kali, na kuziba kwa pua.
   Dalili zingine ni pamoja na kichwa kuuma, uchovu wa mwili, kupoteza hamu ya chakula na hali ya kuchochota kooni.
Dalili hizi huanza ndani ya saa 16 tokea wakati wa kugusana na virusi au visababishi vya mafua. Na hali huwa mbaya katika kipindi cha saa 24 hadi 72 ambapo virusi huwa vingi katika majimaji yatokayo puani.
Katika kipindi hiki mgonjwa wa mafua huwa na uwezo mkubwa wa kuambukiza watu wengine. Dalili za ugonjwa wa mafua hutegemea zaidi uwezo wa mwili wa kupambana na magonjwa kuliko uwezo wa virusi kushambulia nyama za mwili katika njia ya mfumo wa hewa.

Mafua yanaweza kusababisha matatizo makubwa katika mfumo wa kupumua hasa pale yanapoambatana na uambukizo wa pili wa bakteria. Matatizo yanaweza kuwa makubwa zaidi kwa watoto wachanga, wazee au kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini.
Mafua pia yanaweza kusababisha ugonjwa wa uambukizo wa bakteria katika matundu ya fuvu la kichwa (sinusitis), uambukizo katika masikio na koo.
Na katika kipindi hiki mgonjwa hutoa makohozi au makamasi yenye rangi ya njano yanayofanana na usaha. Katika hatua hii, mgonjwa wa mafua anaweza kupata homa kali sawa na mtu mwenye homa ya Malaria.
Kimsingi mafua yanasababishwa na uambukizo wa virusi vya mafua. Wataalamu wa maswala ya afya na tiba wanasema kuwa, kuna aina zaidi ya 200 za virusi vinavyosababisha mafua ingawa virusi aina ya rhinoviruses vilivyogunduliwa miaka ya 1950, ndivyo vinasababisha mafua kwa kwa asilimia 30 hadi 80.
Aina zingine za virusi vya mafua ni human coronavirus, influenza viruses, adenoviruses, human parainfluenza viruses, human respiratory syncytial virus, enteroviruses  na metapneumovirus.
Mara nyingi mtu anaweza kupata uambukizo wa virusi vya mafua vya aina mbalimbali kwa kipindi kimoja anapoumwa mafua.
  Kwa kawaida mafua hutokea zaidi wakati wa mvua na baridi kali. Hii ni kutokana na uwezo wa virusi wa mafua kusambaa kwa kasi wakati wa baridi. Lakini pia katika kipindi cha baridi kali njia ya hewa katika mfumo wa kupumua, huwa kavu kiasi cha kushindwa kukabiliana na virusi wa mafua kwa ufanisi mkubwa.
 Mafua pia yanaweza kusababishwa na mzio katika mfumo wa kupumua. Utafiti uliofanywa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza, ulionyesha kuwa mafua yatokanayo na mzio katika mfumo wa kupumua huchangia kwa asilimia 14.7 katika mzigo wa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo kutokana na magonjwa ya mfumo wa kupumua.
Sababu kubwa zinazochangia kutokea kwa aina hii ya mafua ni uchafuzi wa hewa, vumbi hasa la ndani ya nyumba, moshi wa sigara, hali ya baridi na matumizi ya pafyumu zenye harufu kali.
    Kwa kawaida mafua yatokanayo na mzio hayaambatani na homa, yanakuwa meupe, mepesi, wakati mwingine yanaambatana na muwasho wa macho, ugonjwa wa pumu au kutokea kwa uvimbe wa vinyama puani (nasal polyps).
Katika utafiti ulioongozwa na Zitta J na kuchapishwa katika jarida la Chama cha Madaktari cha Marekani (AMA) toleo la 288(23), ilibainika kuwa watu wanaosafiri kwa ndege kwa muda mrefu kuanzia saa moja na kuendelea, wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa mafua.
Sababu ya jambo hili kwa mujibu wa utafiti huo ni kwamba, kinga ya miili ya abiria wa ndege dhidi ya mafua (mucociliary clearance system) huparaganyika kutokana na ukavu wa hewa ndani ya ndege. Unyevu wa hewa katika ndege inayosafiri zaidi ya saa moja hupungua kufikia kiasi cha asilimia 10 hadi 5.
Ukavu wa hewa au kupungua kwa unyevu katika hewa, husababisha vinywele (cilia) katika njia ya hewa kushindwa kukamata virusi vya mafua na kuvisafirisha hadi tumboni ambako kwa kawaida huunguzwa kwa tindikali (acid) ya tumboni na kufa. Mwili wa binadamu hufurahia na kuwa katika hali bora  pale unyevu wa hewa unapokuwa kati ya asilimia 20 na 60.
   Njia zinazosaidia kukabiliana na tatizo la mafua ni pamoja na
    kunawa mikono mara kwa mara na  
    kuepuka kushika shika pua na macho.
    Ni vizuri kufunika pua na mdomo kwa kitambaa wakati wa kupiga chafya
atika utafiti wao wataalamu wa Chuo kikuu cha Carnegie Mellon waligundua kuwa watu wenye telomere ndefu katika vinasaba vya seli zao aina ya CD8CD28, wana uwezo mkubwa wa kudhibiti virusi vinavyosababisha mafua.
Utafiti huo uliongozwa na Shaldon Cohen na kuchapishwa katika jarida la Chama cha Madaktari wa Marekani (JAMA), Februari 2013.
    Tafiti kadhaa pia zinaonyesha kuwa watu wanaofanya mazoezi ya mwili mara kwa mara, hawakabiliwi na tatizo la mafua mara nyingi ikilinganishwa na wale wasiofanya mazoezi.

Nini kifanyike sasa kupunguza tatizo au kutibu tatizo na ushauri
  WhatsApp 0684127127-0762 986 021

Post a Comment

Translate