Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

Uhusiano kati ya kundi ya kundi la damu(blood group) na uchumba/Mimba/Ujauzito/ mtoto



 
Afya na uchumba na Kundi la damu




1. Binadamu ana damu ambayo ina seli nyeupe, chembe sahani na sell nyekundu.. hizi seli nyekundu ndio zinabeba oksijeni na kabondayoksaidi na kimiminika chenyewe

2. Seli nyekundu zina protini inajishika ukutani mwake inaitwa antijeni (antigen).
kuna antigen A au B au seli inakuwa haina antigen

Ambaye seli nyekundu zina antigen A, ana blood group A.

Ambaye seli nyekundu zina antigen B ana blood group B.

Ambaye seli zake zina Antigen A na B ana blood group AB .

Ambaye seli nyekundu hazina antigeni ana blood group O.


3. katika seli hiyo nyekundu ikiwa na protini inayojishika katika ukuta wake, hii inaitwa D antigen maarufu kama Rh Factor.
Rhesus (Rh) Ni protini inayopatikana kwenye seli nyekundu za damu.
3. a.      Mtu mwenye D antigen katika cell zake nyekundu, blood group yake inaandikwa na kuongezewa alama ya (+)mfano A+, B+, AB+ au O+




3. b.     Mtu ambaye cell zake nyekundu hazina hii antigen D, blood group yake inaandikwa na alama ( -) mfano A-, B-, AB- au O-

4. Hii alama ya (+) au (-) inapatikana je?
4. a.     Baba hutoa Rh moja kwa mtoto, inaweza kuwa Rh+ au Rh- na mama hutoa Rh moja inaweza kuwa Rh+ au Rh-
4. b.     mtoto akizaliwa akiwa na Rh - manake baba alitoa Rh- na mama alitoa Rh -
4. c.   Mtoto akiwa Rh+ anaweza kuwa baba alitoa Rh+ na mama alitoa Rh+
mtoto mwenye Rh + anaweza kuwa alipata Rh- na 5.  d. Rh + ila hatuandiki Rh+Rh- kwa sababu Rh- ni kama haipo.




5. UCHUMBA NA KUZAA /UJAUZITO

Mvulana akiwa na damu yenye (+) ( mfano  A+, B+, AB+ au O+ )
Anaweza kuoana na msichana yeyote mwenye damu group yenye + ( mfano A+, B+, AB+ au O+ ) na watapata watoto bila tatizo lolote.

6. Mvulana akiwa na group mfano ( A+, B+, AB+ au O+) akioa msichana mwenye A-, B-, AB- au O-
6. a. Mtoto wa kwanza atazaliwa vizuri, na ikitokea MSICHANA AMEJIFUNGULIA NYUMBANI au NJE YA HOSPITALI, ambako hakugundulika kwamba ana damu negative... Mtoto wa kwanza ataishi vizuri kabisa na afya nzuri. ila watoto wanaofata hawataweza kuishi au watakufa kabla hawajazaliwa kwa sababu.
6. b. Msichana mwenye negative blood group ( Rh-) yaani hana D antigen, alipojifungua mtoto wa kwanza mwili wake unakuwa sasa umeandaa kujikinga (antibodies kupambana na D antigen ( Rh +) kwa baadae.
MTOTO WA PILI akitungwa mwili wa mama tayari una Antibodies dhidi ya Rh+ ( mtoto anazo hizi Rh+), hivyo matokeo yake ni kuwa seli nyekundu za mtoto zitashambuliwa na kufa.
Mtoto akibahatika kuzaliwa hai, atapoteza uhai muda sio mrefu kwa vile anakuwa hana seli nyekundu za kusambaza damu mwilini.



7. Endapo Msichana huyu alijifungulia MTOTO WA KWANZA HOSPITALI, madaktari wanakuwa wameshajua kwamba ana damu negative, hivyo wanasaidiana na mmewe kufanya maandalizi ya sindano yenye dawa ( SIITAJI HAPA )
alafu msichana akijifungua tuu MTOTO WA KWANZA anachomwa hiyo sindano
na akija kupata mimba baada atachomwa hiyo sindano wakati wa mimba na pindi anapojifungua.

Mtoto mwenye Rh (+) aliyezaliwa na mama mwenye kundi la damu yenye Rh (-)  mama anatakiwa kumchoma sindano ndani ya massa 72 baada ya kujifungua ili kumlinde kwa ujauzito mwingine

Kumb.
Mama akishagundua kwamba kundi lake la damu ni Hasi (-) (A-, B-, AB-, O-) na baba ana kundi lolote ambalo ni chanya (+) Anashauriwa kuchomwa sindano akiwa mjamzito kwenye wiki la 28 na wiki la 34 akiwa mjamzito.

Kwa ushauri zaidi 
Well Dispensary
Whatsapp +255676127127
                   +255743127127

Post a Comment

Translate