JE KUNA ATHARI YOYOTE KWA MTOTO ANAYENYONYESHWA NA MAMA ANAYE KUNYWA POMBE.
Mama anaye nyonyesha sio salama kwa afya ya mtoto mchanga. Maendeleo na ukuaji wa mtoto kiakiri na mwili
Pombe hupatikana kwenye damu na maziwa ya mama ndani ya masaa 2 Hadi masaa 4 kutegemea na kiasi cha pombe mtumiaji alichotumia kwa siku.
Kiasi cha pombe kinaweza kuonekana kwenye maziwa baada au ndani ya dakika 30 Hadi masaa 3.
Kadri kiasi cha pombe kinavyokuwa kikubwa zaidi ndivyo muda wa pombe kuongezeka kubaki kwenye maziwa ya Mama.
Matumizi ya pombe kwa wingi hupunguza uzalishaji wa maziwa kwa ajili ya mtoto na hii huweza kupelekea mtoto kupata maziwa kidogo isivyo kawaida (kukosa chakula cha kutosha na kupelekea afya ya mtoto kuwa duni/ dhaifu).
Adhali za pombe kwa mtoto
Huathiri ukuaji wa akili wa mtoto.
Huathiri maendeleo ya mtoto.
Mtoto kuwa na tatizo la usingizi (kukosa usingizi ).
Mama anaweza kukaa Masaa 2 na kuendelea baadae ya kunywa pombe ndio achukue maamzi ya kumnyonyesha mtoto.
Mama anapotoka kunywa pombe muda mchache na kuanza kumvyonyesha hii huongeza uwezekano wa kumuathiri mtoto.
Ni Baada ya muda gani mama anatakiwa kusubiri ndio amnyonyeshe mwanae Baada ya kunywa pombe.
Chupa 1 ya pombe mama anatakiwa kukaa Masaa 2-3 baada ya kunywa pombe ndio amnyonyeshe mtoto wake
Chupa 2 za pombe Mama anakaa masaa 4 Hadi masaa 5 toka ametoka kuywa
Chupa 3 za pombe Anakaa masaa 6 Hadi masaa 8 ndio amnyonyeshe mtoto wake.
Post a Comment