Je wajua kuna madhara gani kwa mtoto mchanga kutopata maziwa ya mama tu ?
Mama anapojifugua anashauriwa kumnyonyesha mtoto maziwa yake tu ndani ya miezi Sita (6) bila kumchanganyia kitu kingine.
Mama anashauria kumnyonyesha mtoto sio chini ya dakika 30
Unashauriwa kumnyonyesha mtoto maziwa (matiti) yote ili kumsaidia mtoto kupata lishe ya kutosha
Kuna faida zipi pengine ambazo mama na mtoto
Husaidia mtoto kupata virutubisho vyote muhimu kwa afya na ukuaji wa mtoto
Husaidia kutengeneza urafiki na upendo kati ya mama na mtoto
Humsaidia mama kumkinga na saratani ya matiti
Unyonyeshaji mzuri Wa mama humsaidia kutopata ujauzito ni kuwa na maana kwamba hutumika kama njia ya uzazi wa mpango kwa mama
Humlinda mtoto dhidi ya magonjwa kadha wa kadha kama kuharisha
Husaidia mama kurudisha tumbo lake kurudi kwenye hali yake ya kawaida kama awali
Humlinda mtoto asipate ulemavu au udumifu (kudumaa) wa akiri
Humsaidia mtoto kukua na kuwa na afya bora
Matatizo yapi ambayo mama na mtoto anaweza yapata kama hata nyonya maziwa ya mama?
Husababisha mtoto kukosa afya bora na kumfanya kupata utapiamlo
Hupunguza urafiki na upendo kwa mtoto na mama
Humweka mama kwenye hatari ya kupata ujauzito ndani ya muda mfupi
Husababisha mtoto kudumaa kiakiri na afya mbaya.
Humpelekea kwenye hatari ya mama kupata saratani ya matiti na maziwa kuvimba au kujaa
Ahsante
Kama umependa makala hii Tafadhali usisahau kutoa maoni yako pamoja na ushauri
Pia kama unaswali Unaweza kututafuta kwa WhatsApp no. 0684127127
Post a Comment