SARATANI /KANSA
SARATANI / KANSA
Ni Ugonjwa unaotokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika na hivyo hazipo katika hali yake ya kawaida.
Note: Saratani inampata mtu wa Aina yoyote yule.
VITU VINAVYO PELEKEA MTU KUPATA SARATANI / KANSA
- Uvutaji wa sigara
- Unywaji wa pombe
- Umri kuwa mkubwa >50 miaka
- Kuridhi
- Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 16)
- Kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja
- Maambukizi ya virusi vya HPV (Human papillomavirus)
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
- Umri zaidi ya miaka 50
- Upungufu wa kinga mwilini (VVU/UKIMWI)
- Kupata mimba katika umri mdogo
- Idadi kubwa ya watoto na kuzaa mara kwa mara
- N.k
Mtu anaweza kupata saratani moja au zaidi ya zifuatazo.
Zifuatazo ni baadhi ya saratani ambazo mtu anaweza zipata.
- Saratani ya Ubongo
- Saratani ya Koo
- Saratani ya Damu
- Saratani ya Mapafu
- Saratani ya Matiti
- Saratani ya Ini
- Saratani ya Tezi dume
- Saratani ya Ngozi
- Saratani ya Damu
Saratani ya koo.
- Chakula kukwama kwenye koo
- Siku za mwanzo mgonjwa anaweza kushindwa kumeza chakula kigumu kisha cha majimaji na baadaye akashindwa kumeza hata mate
- Maumivu wakati wa kumeza chakula hasa chakula kigumu
- Maumivu kwenye kifua au mgongoni
- Kupungua uzito
- Kiungulia
- Sauti ya mkwaruzo au kikohozi kikavu cha zaidi ya wiki mbili
- Saratani ya shingo ya kizazi.
- Kulalamika maumivu ya tumbo chini ya kitovu
- Kutibiwa kwa dawa za kumeza na kuweka ukeni kwa muda mrefu bila kupona au nafuu
- Kupoteza hamu ya tendo la ndoa
- Kutokwa na maji maji ukeni yenye harufu
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
Mfumo mpya unaokuwezesha kujipatia kipato chako hapo hapo ulipo bila kuwa na mtaji mkubwa soma hapa http://afyateam.blogspot.com/2018/01/mfumo-mpya-unaokuwezesha-kujipatia.html
Saratani ya tezi Dume.
- Kupoteza hamu ya tendo la ndoa
- Korodani kuuma
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Tezi kuvimba
- Shida ya kukojoa
- Maumivu
Saratani ya INI.
- Macho na ngozi kuanza kubadilika na kuwa na rangi ya njano
- Uchovu,
- Hisia ya uvimbe katika ini (au uboreshaji wa tumbo);
- Uvimbe wa miguu
- kutokwa damu kutoka pua;
- kichefuchefu, kutapika;
- Joto la juu;
- Matatizo ya tumbo, ugonjwa wa
- kupungua, kuhara;
- kupungua uzito;
- Ascites au tumbo kujaa maji(hatua za hatari).
Saratani ya Ngozi.
- Ngozi kuanza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu-nyeusi na nk
- Kuanza kuvimba kusiko eleweka kama vinundu kwenye ngozi
- Ngozi inaweza kuanza kuwasha na maumivu wakati mwingine
- Tezi zilizo karibu na sehemu iliyo adhiriwa kuvimba
Saratani ya Ubongo.
Sehemu ya mbele (frontal)
- Kuumwa na kichwa
- Ulegevu mwilini
- Kufa ganzi sehemu moja ya mwili
- Mabadiliko ya haraka mwilini,hisia ,moyo na tabia
- Kuchanganyikiwa na akili
Sehemu sawia (parietal)
- Kuumwa na kichwa
- Kushikwa na kifafa
- Kufa ganzi
- Shida unapoandika hati
- Shida unapojaribu kusonga kwa namna Fulani
- Shida kufanya hesabu rahisi
Sehemu ya nyuma (occipital)
- Kuumwa na kichwa
- Kushindwa kuona vizuri
- Kuona mazingaombwe yako tu
- Kushikwa na kifafa
- Kwa muda mfupi (temporal)
- Kuumwa na kichwa
- Kushikwa na kifafa
- Shida ya kufuata maagizo kwa pamoja
- Kutong’amua usumbufu wa hali ya anga.
Saratani ya Mapafu.
- Kikohozi cha Mara kwa Mara
- Kupata shida ya kupumua
- Kupunguza uzito
- Kukohoa damu
Saratani ya Damu.
- homa au baridi;
- uchovu sugu na udhaifu;maambukizi ya mara kwa mara au kali;
- kupoteza uzito usiojulikana;
- vidonda vya lymph zinazowaka, ini au ukubwa;
- Tabia ya kutokwa na damu na kuvunja;
- kutokwa damu mara kwa mara kutoka pua;
- kuonekana kwa dots nyekundu kwenye ngozi (petechia);
- kuongeza jasho, hasa usiku;
- Maumivu mifupa;
- Udhaifu wa mifupa.
Saratani ya matiti.
- Uvimbe kwenye matiti au kwapa
- Mabadiliko katika umbo la matiti
- Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo
- Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje
- Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa
- Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura
Nini cha kufanya uonapo dalili hizo wahi kituo cha afya kwa uchunguzi na Huduma ya matibabu
Usiache kutoa maoni yako hapa chini
Afya online
Tunajali afya yako.
Tunajali afya yako.
Post a Comment