Slider


Sports

Life & style

Comments

Fashion

Technology

Blogroll

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo pamoja na magonjwa mengine mwilini.

 Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya. Ukipatwa muda mrefu au kila wakti ; basi …chunguza zaidi.

Kichomi husababishwa au kinaweza kuwa.

• Dalili ya matatizo ya tumbo lenye asidi (acid) kuzidiDalili za ugonjwa wa moyo uitwao Ischemic

Jambo la kuangalia ni je?

• Unashikwa kichomi ukiwa unatembea?• • Umeinama au umelala

• Ukishakula chakula


Kama unapatwa kichomi wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali ina manisha kuwa  

• kuna tatizo la damu kuingia sawasawa au kuzunguka (circulation) katika moyo.


Kama unapatwa kichomi baada ya kula ina manamanisha

•  kuna tatizo katika chakula unachokula. • Je mlo wako una acid(uchachu) sana? • • Je, unakula vyakula vyenye pilipili na binzari(spices) kwa wingi sana? 

Kama una kula sana vyakula vyenye asidi ina maana tumbo lako halimeng’enyui sawasawa linachoka.

Kawaida binadamu unabidi kubadili badili ulaji. Usirudie vitu fulani fulani kila siku. Mathalan usiweke pilipili kwenye chakula.


Tatizo ni ulaji wa chakula chenye chumvi nyingi sana. Chumvi inakorofisha pia mzunguko wa damu mwilini.

Hasa kama hunywi maji.


Kama unapatwa kichomi ukiwa umelala au umeinama 

• Hii ina manisha kuwa kuna tatizo pia la mzunguko wa damu ndani ya moyo au kwenda moyoni. 

• Labda una tatizo la unene (je unafanya mazoezi ya kutosha?) kama unafanya mazoezi, je unafanya mazoezi ya aina gani?

Kuna mazoezi ya aina mbili.

• Mazoezi ya nguvu na haraka (cardio vascular); kama kukimbia, mpira, ngumi, kuinua vyuma nk.

• Mazoezi laini yanayofanywa kwa kukihimili (isometric) mathalan ukiweka mkono upande mmoja wa kichwa huku ukisukuma kichwa kisukumane na mkono, unafanya tizi la kuongeza nguvu ya shingo. Zoezi aina hii linaitwa Isometric.

Aina ya mazoezi ya aina hii ni kama Yoga, Pilates na baadhi ya mitindo mbalimbali ya mapigano yaani masho ati mathalan Tai Chi ya Kichina.

Tizi la Yoga zuri sana maana limetulizana:

Pilates si tofauti sana na Yoga ni kama ndugu wa karibu. Ila Pilates inafafanua zaidi mambo mengine kama tumbo nene:

 Sio muhimu kuchanganya mazoezi haya mawili. Yaani ukishafanya mazoezi ya nguvu, ya kuhema unatulizana.

Kama una kichomi cha mara kwa mara yaweza kuwa ni dalili za ugonjwa wa moyo, kisukari au mambo mengine. Kuondokana na mambo haya:

Kamwone mganga wa moyo Kama huna ugonjwa wa moyo angalia vyakula unavyokula. 

• Je, unakula sana vyakula vya mafuta

• Punguza ulaji wa mafuta au vyakula vizito jaribu kula zaidi samaki ambao huwa na mafuta yasiyoumiza mwili.

• VITUNGU SAUMU VIBICHI vinasaidia sana kukinga moyo, matatizo ya mafuta, lakini tatizo ni harufu mbaya ya mdomo.    Hivyo unaweza kuwa unachanganya na mboga nyingine za saladi unapokula mlo kila siku. Kama nyanya, matango, nk.

• Mbali na ulaji suala la mapumziko ya kutafakari au kwa kimombo Meditation limefanyiwa utafiti na kuonekana kwamba linasaidia sana maradhi ya moyo, akili na “stress” ya mwili kwa ujumla. Jaribu hizi hapa chini, ukiweza dakika kumi hadi 20; mara mbili kwa siku, kufuatana na muda ulio nao.

1.KUKAA TU

2. KUVUTA PUMZI

3. KULALA CHALI HUKU UNAVUTA NA KUPUMU hii ni aina ya masho ati ya Kirusi ambayo inasisitiza Uvutaji pumzi sahihi. Inaitwa Systema.

Mazoezi Haya yanaweza kukusaidia pia

  https://youtu.be/h9uxH_S2vfc

Karibu kwa maswali

Post a Comment

Translate